Home Mchanganyiko TASAF Yawanusuru Wanafunzi na Shambulio la Simba Ludewa

TASAF Yawanusuru Wanafunzi na Shambulio la Simba Ludewa

0

Wakazi wa Kijiji cha Ngalawale kilichopo wilayani Ludewa mkoani Njombe walilazimika kuunganisha nguvu na kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya msingi Ngalawale kwa kujenga vyumba vitatu vya madarasa na nyumba moja ya mwalimu ili kuepusha hatari ya watoto kuliwa na wanaya wakali wakiwemo Simba pamoja na mimba za utotoni kwasababu ya kusafiri umbali wa zaidi ya km 9 kufata elimu katika shule ya msingi Songambele na ludewa kijijini.

Mara baada ya kukamilika vyumba vitatu wakaomba serikali kuruhusu shule hiyo kuanza kutumika bila kukamila usajiri sambamba na miundombinu mingine ,nia ambayo ikaigusa serikali na kuamua kuwasapoti wananchi hao kwa kujenga vyumba vinne vya madarasa pamoja na jengo la utawala kupitia mradi wa TASAF ili kuharakisha dhamira ya kusogeza huduma ya elimu kijijini hapo na maeneo jirani.

Winfred haule na Matha Benard ni wakazi wa Kijiji cha Ngalawale wakieleza hali ilivyokuwa kwa watoto kabla ya kuanzisha shule hiyo wanasema wanafunzi walikuwa katika hatari ya kushambuliwa na simba na fisi ambao wanatoka hifadhi ya SEREOUS na kuvamia maeneo ya makazi ya watu hivyo kuanzishwa kwa shule hiyo kumenusuru maisha na mimba za utotoni zinazosababishwa na kutembea umbali mrefu katika mabonde na milima.

Wanasema hatua iliyofikiwa itakuza kiwango cha ufauru na taaluma kwa ujumla wilayani Ludewa kwa kuwa watoto wamepunguza utoro. ili kuwahi nyumbani.

Lakini licha ya shule hiyo yenye madarasa matatu na walimu 3 tu, kuanza kutoa elimu ikiwa haijapatiwa usajiri huku miundombinu ikiwa bado duni inaibua hisia kwa mwalimu mkuu Betrice Mtweve ambaye anatumia fursa hiyo kuiomba serikali kuharakisha usajiri ili iweze kupata mgao wa fedha za elimu ili kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya kutoa elimu ikiwemo ujenzi wa Nyumba ,vyoo na madarasa.

Nae mratibu wa TASAF wilayani Ludewa William Malima anasema serikali baada ya kuona jitihada za wananchi walikubaliana kutoa michango ya hali na mali na kufanikisha ujenzi wa majengo matatu ikawiwa kuwaongezea nguvu kwa kuwajengea madarasa mengine 5 ili kukamilisha mradi huo ambao umekuwa neema kwa watoto

Katika mkoa wa Njombe TASAF inatekeleza miradi yenye thamani ya bil 13.2 huku ludewa miradi yake ikiwa Ni 36 yenye thamani ya bil 1.7.