Home Mchanganyiko WAHITIMU WA VETA CHANG’OMBE WAASWA KWENDA KUONESHA UJUZI WAO KATIKA SEKTA YA...

WAHITIMU WA VETA CHANG’OMBE WAASWA KWENDA KUONESHA UJUZI WAO KATIKA SEKTA YA VIWANDA

0

Meneja wa Uajiri wa Kioo Limited Jacob Msuya akizungumza na waandishi habari katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe  yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Chang’ombe Vaileth Fumbo akizungumza katika mahafali ya 49 ya chuo kuhusiana na historia ya uzalishaji wa ujuzi wenye mafanikio yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Wahitimu wakionesha vipaji vyao uimbaji katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahitimu wa fani ya ubunifu wa mitindo ya nguo wakiimba wimbo wa Taifa mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Rais wa Serikali ya Wanafuzi wa VETA Chang’ombe Nurdin Chambalini akitoa ushauri kwa wahitimu katika kwenda kutekeleza dhana ya Rais Dkt.John Magufuli ya ujenzi wa viwanda.

*****************************************

Wahitimu wa vyuo vya Ufundi Stadi wameaswa kutumia taaluma zao katika kutengeneza ajira kutokana na ujunzi wao kwani serikali iko katika mkakati wa kwenda uchumi wa kati wa viwanda.

Akizungumza na katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Chang’ombe Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Meneja Uajiri wa Kioo Limited Jacob Msuya amesema kuwa wahitimu wana kila sababu ya kwenda kuongeza fursa za ajira kwa kutumia mafunzo walioyapata.

Msuya amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kuwa na ueledi wa kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu wa baadhi ya vitu kutokana na taaluma walioipata katika Chuo cha VETA Chang’ombe.

Aidha amesema kuwa wahitimu wa VETA wamekuwa wakifanya vizuri kwani Kioo Limited kimepata kufanya kazi na wahitimu na wengine kuwaajiri katika kiwanda.

“Ninategemea baada ya kutoka hapa watakwenda kuleta matokeo ya taaluma walioipata kwa kufanya kazi kwa bidii na sio kuwa na cheti kisichokuwa na kazi ilhali kuna watu waliwekeza katika kuhakikisha kijana wao ana ujuzi wa kwenda katika ajira au kujiajiri na kujiletea maendeleo”

Amesema viwanda viko vichache ikilinganishwa na wahitimu katika vyuo mbalimbali  vinaendelea kujengwa kutokana serikali kuwa na mkazo katika sekta ya viwanda hivyo vijana lazima wapambane katika suala la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa.

Nae Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Chang’ombe

Vaileth Fumbo amesema wahitumu katika mahafali ya 49 wako 556 ambapo kazi yao kubwa ni kuwenda kutumikia taifa kwa ujunzi waliopata katika kipindi cha miaka miwili.

Amesema kuwa wahitimu waende na mfumo wa kuanzisha kikundi ambapo wanaweza kuanzisha kiwanda na taasisi fedha kuwakopesha katika kiwanda ambacho wamekianzisha.

Fumbo amesema wasibweteke na vyeti  kwani ndio mwanzo kwenda mbali zaidi kwa kuongeza ujuzi katika kutanua uwigo wa ajira au kujiajiri.

 

Rais wa Serikali ya Wanafuzi wa VETA Chang’ombe Nurdin Chambalini amesema kuwa watanzania wajue kauli ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ya Viwanda hivyo wahitimu wakaendeleze kauli hiyo katika ujenzi wa viwanda.