Home Michezo SIMBA FC YAAMBULIA KIPIGO KWA MWADUI FC, SHINYANGA.

SIMBA FC YAAMBULIA KIPIGO KWA MWADUI FC, SHINYANGA.

0

********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imeambulia kipigo cha 1:0 na Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Mwadui FC ilipata bao hilo kupitia kwa nyota wao Gerrald
Mathias mnamo dakika 33′.

Katika kipindi cha pili Klabu ya Simba ilionesha kila dalili kuweza kurudisha bao hilo hasa kwakumiliki mpira kwa asilimia kubwa bila mafanikio.

Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi mchezo ulibaki kwa kuwapa faida klabu ya Mwadui Fc kwa goli hilo lilodumu kwa muda mrefu.

Matokeo haya yanaifanya Simba ipoteze kwa mara ya kwanza msimu huu lakini ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama zake 18.