Home Michezo SADNEY URIKHOB AING’ARISHA YANGA UGENINI MECHI YA LIGI KUU

SADNEY URIKHOB AING’ARISHA YANGA UGENINI MECHI YA LIGI KUU

0

Na.Mwaandishi Wetu,Mwanza

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga, Sadney Urikhob ,ameing’ara ugenini timu ya Yanga kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Mbaon FC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Yanga wamepata ushindi wa pili mfululizo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania wakitoka kuifunga Coastal Union bao 1-0.

Kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu huku David Molinga akiwa ameikosesha Yanga mabao mawili ya wazi.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo Yanga walinufaika kwa mabadiliko hayo na kuweza kupachika bao lililofungwa na Sadney Urikhob,akimalizia krosi ya Kiungo Mshambuliaji Mapinduzi Balama.

Kwa Matokeo hayo Yanga wamefikisha pointi 7 huku wakiwa wamecheza mechi nne kushinda miwili,sare moja na kufungwa moja.