Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania
Dkt. Alex Mubiru kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-
Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Wengine
katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia,
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kulia,
Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey
Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe pamoja na viongozi
wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea nje ya lango kuu ya
Stendi hio ya mabasi kuzungumza na wananchi mara baada ya
kuifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya
kufungua stendi hio ya mabasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Meneja Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa barabara
ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na Wakandarasi, Wahandisi Washauri wa miradi ya barabara ya Tabora-
Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya
Mpanda mjini mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe mara baada ya
kuzindua na kufungua miradi ya barabara mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania
Dkt. Alex Mubiru, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Agrey Mwanri kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa
mradi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi
zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth
Magufuli pamoja na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa Stendi Kuu ya Mabasi Mizengo Pinda nje kidogo ya Manispaa ya
Mpanda mkoani Katavi.
Sehemu ya Barabara ya Mpanda –Stalike iliyokamilika
kujengwa kwa kiwango cha lami.
PICHA NA IKULU