Home Mchanganyiko SUMA JKT YAKABIDHI JENGO LA MADINI KWA WIZARA YA MADINI KAGERA.

SUMA JKT YAKABIDHI JENGO LA MADINI KWA WIZARA YA MADINI KAGERA.

0

Jengola Madini ambalo limekabidhiwa Suma Jkt kwa Wizara ya Madini

Wafanya kazi wa Suma JKT,Waziri wa madini Mh.Doto Biteko,Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia General Marco Gaguti,katibu Tawara wa Mkoa na viongozi wengine wa wizara hiyo wakipata picha ya pamoja baada Wizara ya Madini kuimekabidhiwa jengo la madini na SUMA JKT Mkoani Kagera.

************************

 

Na Silvia Mchuruza;

Bukoba;

Wizara ya madini kupitia kwa Waziri wa madini nchini Mh.Doto Biteko  imekabidhiwa jengo la madini na SUMA JKT  ambalo pia litakuwa linatumiwa na wachimbaji wadogo wadogo ambapo waziri amesistiza mikoa iliyoko pembezoni kuondoa vikwazo kwa wachimbaji wadogo  wadogo na  wasafirishaji wa madini ambao wanasafiriha sampuli za madini kutoka nchi nyingine.

Alitoa kauli hiyo akiwa mkoani Kagera wakati akikabidhi kituo cha umahiri wa shughuli za madini ambapo kituo hicho kitatumika katika shughuli mbalimbal za kuwasaidia wachimbaji  wadogowadogo kuapata elimu ya ufanisi juu ya uchimbaji wa madini mbalimbali.

 

Katika makabidhiano ya kituo hicho alimweleza mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia General Marco Gaguti  kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya watendaji ambao wanahusika katika sekta za ukaguzi wa madini kuwakwamisha wadau mbalimbali ambao wanakujana sampili zao kupima katika maabara zilizoko nchini jambo ambalo linasababisha upotevu wa fedha  katika mikoa husika.

 

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi,kinachonisikitisha ni kupiga fedha teke ambazo zingechanga uchumi wetu kwani kama kutakuwa na udhoroteshaji kwa mtu yeyote aliyefata vigezo vya kuleta sampuli zake huo uchumi wa kati tutachelewa kuufikia,ombi langu ni kuona mikoa ambayo ipo pembezoni  inaondoa vikwazo hivyo vyenye dalli za Rushwa ili kurahisisha uchumi wetu,alisema Biteko.”

 

Ametaja katika mkoa wa Kagera mipaka inayokwamisha wadau mbalimbali wanaoleta sampuli zao kuwa ni Mipaka ya Kabanga,Rusumo,Mtukula ambapo watendaji hao wamekuwa na visingizio mbalimbali na kukwamisha wafanyabiashara hao takribani siku 5 hadi 7  huku akiutaka uongozi wa mkoa kukabiliana na changamoto hiyo.

 

Aidha alisema ili kukabiliana na changamoto ya mbalimbali katika skta ya madini na kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika tayari lesseni 12,000 nchini  zilizokuwa zimewekwa mfukoni mwa watu waliokuwa hawajishughulishi na uchimbaji zimefutwa huku mkoa wa Kagera  ukifutiwa lesseni 156 ili kutoa fursa kwa wachimbaji kutumia kituo kipya kuomba lesseni za uchimbaji.

 

Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho cha Umahiri  ambao ni miongoi mwa majengo saba ambayo yamejengwa Songwe,Musoma,Bariadi,Chunya,Handeni,Bukoba na Tanga Enjinia Fabiani Buberwa Meneja wa SUMA JKT kanda ya ziwa amesema majengo yote hayo yamesimamiwa na SUMAJKT ambapo yamegharimu kiasi cha shilingi billion 3.

 

Alisema SUMAJKT itaendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na kuokoa fedha ili kujenga majenga yenye tija ambayo yatawezesha wananchi kupata maendeleo na huduma karibu ili kuunga mkono azima ya serikali ya kutetea wananchi wanyonge.

 

Kufuatia changamoto zinazojitokeza mpaka mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia General Marco Gaguti ametoa wiki moja kwa Afisa madini mkazi kuandaa mkutano ndani ya wiki moja ambapo anapaswa kuhakikisha mkuu wa mkoa na katibu tawala wa mkoa wa Kagera wanakutana na watendaji wanahohusia mipakani ili kufuta ufumbuzi wa pamoja ambao utaondoa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya madini.