Home Mchanganyiko TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WIKI YA UTUMISHI...

TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

0

TANGAZO

 

            MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA
UMMA

 

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17
hadi 22 Juni 2019
.
Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya
Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali
zinazohusu Utumishi wa Umma.

 

Wakati wa maadhimisho hayo,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa madawati
maalum ya kutoa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya
Mtumba jijini Dodoma na zile zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

 

Huduma zitakazotolewa ni
pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa hoja mbalimbali za wananchi kuhusu
Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.

 

Madawati hayo yatakuwa wazi
kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.

 

NYOTE MNAKARIBISHWA.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

14 Juni 2019